"Habari zilizopewa uzito"
Habari Mbali mbali

MAKAMU WA RAISI WA TANZANIA AJIONEA ATHARI ZA MAFURIKO DAR..........!!!


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe, sehemu ya Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, wakati Makamu alipofanya ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo Aprili 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wanaosimamia shughuli ya daraja hilo, baada ya kuwasili eneo hilo leo.
ehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja.
Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo, katika eneo la Daraja la Mpiji, linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, leo Aprili 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Share and Enjoy:

0 comments for this post

Leave a reply

Pata Habari papo kwa hapo
Weka anuani pepe yako hapa ili upate habari punde tunapo ziweka katika EAfrican Blog!
Subscribe via RSS Feed subscribe to feeds
wadhamini
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Popular Posts
Recent Stories
Ukurasa wetu wa Facebook
Wadhamini
Search
Archives
Blog Archives
Recent Comments
Tag Cloud