"Habari zilizopewa uzito"
Habari Mbali mbali

LHRC J.K KWANINI KUIVUNJA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimestushwa na kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuivunja mapema Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema haikustahili kuvunjwa wakati Bunge Maalumu la Katiba bado linaendelea.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na mjumbe wa Kamati Maalumu ya Katiba kutoka LHRC, Exavery Lwaitama, alipokuwa akitoa mada kwenye warsha ya jukwaa la mchakato wa katiba mpya, ulioandaliwa na Mtandao wa Kufuatilia Sera Mwanza (MPI), na kuwashirikisha viongozi wa asasi na mashirika mbalimbali kutoka wilaya za Ukerewe, Nyamagana, Ilemela, Magu za mkoani Mwanza, pamoja na Wilaya ya Karagwe, Kagera.


Lwaitama ambaye pia ni mhadhiri mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kuvunjwa kwa tume hiyo wakati Bunge la Katiba halijamalizika, ni kuharibu mwenendo na mchakato mzima wa Watanzania kupata katiba wanayoitaka.


Alisema haiwezekani Rais Kikwete aivunje tume hiyo kisha majukumu yake kuchukuliwa na serikali ambayo tangu awali imekuwa ikikataa kutungwa kwa katiba mpya. 
“Utavunjaje tume wakati Bunge la Katiba halijaisha? Sasa hii rasimu ya katiba inayojadiliwa bungeni itasimamiwa na nani kama tume imevunjwa? Itawezekanaje isimamiwe na serikali ambayo tangu mwanzo haitaki kutungwa kwa katiba mpya?

“Tunakumbuka mwaka 2011 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Jaji Fredrick Werema), na viongozi wengine wa serikali walikataa kutungwa katiba mpya. Sasa leo rais anaivunja tume, hivi tunategemea kuna upatikanaji wa katiba hapa?” alihoji Lwaitama.


Wakizungumza katika warsha hiyo, viongozi wa mashirika na asasi hizo, walisema hawaoni mwelekeo wa Watanzania kupata katiba mpya wanayoitaka, hivyo wakasema ni bora Bunge hilo likavunjwa, ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha.


Mratibu wa MPI, Jonathan Kassim, alisema wameandaa warsha hiyo ili kutoa sauti ya pamoja kwa asasi na mashirika hayo kuhusu mwenendo wa Bunge hilo na kuwaomba wajumbe na serikali kwa ujumla kuwatendea haki wananchi kwa kupitisha maoni yao.

Share and Enjoy:

0 comments for this post

Leave a reply

Pata Habari papo kwa hapo
Weka anuani pepe yako hapa ili upate habari punde tunapo ziweka katika EAfrican Blog!
Subscribe via RSS Feed subscribe to feeds
wadhamini
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Popular Posts
Recent Stories
Ukurasa wetu wa Facebook
Wadhamini
Search
Archives
Blog Archives
Recent Comments
Tag Cloud