SPIKA WA BUNE LA AFRIKA MASHARIKI KUPANDISHWA KIZIMBANI
Mgogoro wa uongozi umezuka katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo wabunge wa bunge hilo wanakusudia kumwondoa madarakani spika wa bunge hilo.
Tayari wabunge hao wameshakusanya saini 36 kutoka kwa wabunge 45 wa bunge hilo ambazo zinatakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Wabunge hao wanamlaumu Spika huyo kwa kukiuka kanuni za bunge pamoja kushindwa kuwashirikisha wabunge kwenye baadhi ya uamuzi.
Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa wabunge hao kwa niaba ya wabunge wenzake wa bunge hilo Abudulla Ali Hassani Mwinyi, amesema wabunge hao wamefikia hatua hiyo ya kumwondoa spika huyo Margareth Zziwa kufuatia kukerwa na mwenendo wake.
Tayari wabunge hao wameshapeleka hoja ya kumwondoa spika huyo kwa Katibu wa Bunge hilo ikiwa na sahihi za wabunge 36 ili kutimiza matakwa ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo ili kuanzisha hoja ya kumwondoa spika.
Je wabunge hao hawakuwa na njia nyingine kumaliza mgogoro huo hadi kufikia hatua ya kutaka kumwondoa spika huyo.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo umesababisha kuahirishwa kwa bunge hilo tangu jana kwa muda usiojulikana baada ya spika huyo kuamua kuliahirisha kwa muda usiojulikana.
Hii inafuatia malumbano yalijitokeza ndani bunge hilo ambapo mmoja wabunge alisema hoja hiyo isingeweza kujadiliwa.
BBC ilifanya juhudi za kuwasiliana na spika huyo Margareth Zziwa kwa simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo hata hivyo alikataa kusema chochote ambapo alishauri apigiwe afisa habari wa bunge hilo ili atoe ufafanuzi.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo bado haijajulikana utamalizika lini lakini kwa vyovyote vile utakuwa umeathiri shughuli za Bunge hilo la Afrika Mashariki.
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more great content just like it.
-
Na Yericko Nyerere (Mwanahalisi Forum) Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu a...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Muss...
-
Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambaye T...
-
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na ku...
-
THE Monduli Constituency MP, Edward Lowassa (b. Aug. 26,1953), has been causing a political storm of gargantuan proportions across the Tan...
-
Teller Ref No. UTT -MFI/TL/0414/15 Company:UTT Microfinance Plc Location:Dar Es Salaam POSITION DESCRIPTION: The UTT Microfinance Plc now i...
-
The jet, christened ‘The Great Rift Valley’ is the first of six 787s which Kenya Airways has ordered as part of its mordernisation ...
-
A list of famous people, chosen mainly from the Ninenteenth, Twentieth or Twenty First Century. This list includes famous actors, politici...
-
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimestushwa na kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuivunja mapema Tume ya Mabadiliko ya Katiba n...



0 comments for this post
Leave a reply