"Habari zilizopewa uzito"
Habari Mbali mbali

PROF ISSA SHIVJI NA UBAKAJI WA MATAKWA YA UMMA NA MUUNDO WA MUUNGANO

NA YERICKO NYERERE Nikiwa katika hospitali ya Jeshi la Wanamaji Kigamboni asubuhi ya leo ambapo nimelazwa kwa kuumwa maralia, nimezama kwenye tafakuri, nikiangaza mchakato wa upatikanaji wa Katiba ya Jamhuri ya Watu wa Tanzania, nikajikuta namfikiri Profesa Issa Shivji kwa hadira yake jana mbele ya kikundi kilichojiita cha wasomi wa vyuo vikuu (makada wa ccm). Sijawahi kufundishwa na Profesa huyu anaeishi Amerika akighani sheria zake katika uga wa Pwani ya Azania, nimjenzi mzuri wa hoja za kisheria vilevile jamii ya kiswahili ipo katika hatari kubwa kwakuwa inamuamini mtu huyu kwa misimamo yake, Baada ya Tanzania kuanza mchaato wa kupata katiba mpya ya Muungano, Prof Shivj alikuwa miongoni mwa watu wanaotazamiwa kulisaidia taifa kupata katiba bora kabisa ya "KIRAI", lakini katika hali isiyotegemeka, mamlaka zote za nchi zikamtelekeza, akawa sasa ni deiwaka tu katika msako wa katiba mpya, akionyesha kuheshimu misimamo ya uuma. Mnyukano wa kimaslahi kati ya Chama cha Mapinduzi na UMMA wa Watanzania, umemrejesha tena Issa Shivji mbobevu wa sheria za kiutawala, lakini akija kwa nadharia ya kusigina matakwa ya umma, Yule Issa Shivji aliyekuwa mtetezi wa matakwa ya umma, leo amekuwa mpiga zumari wa Lumumba. Issa Shivji anafikiri Watanzania ni wajinga kiasi cha kumfuata kila akifanyacho, vikao vyake vya ikulu wiki jana kwamalengo ya ghiriba wa umma havita saidia Watanzania kudai Muungano wao BORA kabisa wa Serikali TATU. Hoja za Issa Shivji hazijitoshelezi, na zinajibika kirahisi kama zilivyojengwa kirahisi. Katika kifungu cha 4(2)cha maelezo yake, anasema "katiba ya Zanzibar imeleza na kufafanua kuwa Zanzibar ni dola, kosa liko wapi? Kwanini jambo hilo linakuzwa mpaka kudai kuwa Zanzibar imejitangaza ni nchi?" Katika tafsiri yake binafsi, anataka ineonekane kuwa kilichomaanishwa katika katiba hiyo ni dola, kama ndivyo, kwa nini hata yeye mwenyewe hataki ionekane kuwa Zanzibar imejitangaza ni nchi? Anaendelea kusema kuwa "kama kweli Zanzibar imetangaza kuwa ni nchi basi wangeuandikia umoja wa mataifa(UN) kuwajulisha..." Ina maana kwa profesa huyu, kutoandika barua UN tu ndio uthibitisho tosha kwamba Zanzibar haijajitangaza kuwa nchi? Mbona katika kile kilichoitwa na vigogo ndani ya serikali ya CCM kama "ripoti ya baraza la mapinduzi juu ya matatizo na kero za muungano na taratibu za kuyaondoa ya mwaka 2004" ilipendekeza pamoja na mambo mengine, ushirikiano wa kimataifa usiwe ni suala la muungano. Shivji haoni kuwa hii ni hatua moja ya kuelekea kuwatangazia hao UN kuwa Zanzibar ni soverein state? Katika kipengele kidogo cha 3 anauliza kama ni kweli Zanzibar ina madaraka kamili toka 2010 ni kwa nini badi inadai mamlaka kamili imejibiwa na maelezo hapo juu. 4(4) Profesa Shivji anasema " kama kweli neno nchi maana yake sio dola, basi tujiulize, Rasimu katika pendekezo lake la muundo wa serikali tatu imependekeza nchi tatu?, yaani nchi ya Tanganyika, nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanzania?... inapendekeza dola tatu, ugumu wa kukubali Zanzibar kama dola uko wapi?" Hapa Shivji anachanganya maelezo, na anajiconradict, mwanzo ameeleza kuwa dola ni mjumuisho wa vyombo vitatu, mahakama, bunge na serikali, rasimu imependekeza serikali tatu, hii tafsiri ya ya serikali tatu ni sawa na kusema dola tatu ameitoa wapi? Kama amejitungia tu, kwa nini utetezi wake huu tusiuite ni batili? Anakiri kuwa ni kweli katiba ya JMT inasema kuwa JMT ni nchi moja na Zanzibar ni sehemu yake, lakini badala ya kukiri pia kuwa katiba ya Zanzibar imekiuka katiba ya JMT na kwamba ni batili, anajikita katika kueleza sababu za Zanzibar kukiuka katika ya JMT (ambazo hata hivyo sio za kikatika) kama maelezo yake kuwa maana ya neno nchi kwenye katiba ni dola kwa hiyo katiba ya JMT inavyosema kuwa JMT ni nchi moja, ina maanisha kuwa ni dola moja?, kamandivyo hivyo dola ya Zanzibar inatoka wapi? Katika upunguzaji wa mamlaka ya bunge la JMT shivji anaeleza kuwa kinachozungumzwa na sheria hiyo ni kuwa tabled katika baraza la wawakilishi kwa taarifa na eti haina madhara; Huu sio tu kuwa ni utetezi dhaifu bali pia sio kweli. Yeye mwenyewe Shivji ametoa mifano ya sheria zilizorudishwa katika bunge la JMT ili kufanyiwa marekebisho ndipo zikubaliwe kutumika Zanzibar, utasemaje hakuna madhara?, utasemaje ni kwa ajili ya taarifa tu wakati sheria zinakataliwa? Kuhusu mamlaka ya kugawa nchi katika mikoa na wilaya; Shivji anajenga hoja kuwa; (1)Mambo ya utawala wa mikoa na wilaya yaani serikali za mitaa sio jambo la muungano. Hapa ni dhahiri kuwa mwanazuoni huyu amelenga kupotosha, unasemaje kwamba kugawa nchi katika mikoa na wilaya ni mambo ya utawala wa serikali za mitaa?, yaani ni kuingilia TAMISEMI? Kugawa nchi katika mikoa na wilaya hauhusiani na tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)hivyo huwezi sema kuwa sio suala la muungano. Vilevile Shivji ananukuu katiba ya Zanzibar baada ya mapinduzi, yaani kabla ya katiba ya mwaka 1984 kuwa iliruhusu Raisi wa Zanzibar kugawa maeneo ya Zanzibar, hii hoja ni mfu kwa sababu ndio maana ikabadilishwa. Kitu cha kushangaza ni kwamba Shivji anaona ni sawa tu kwa kuwa Zanzibar imerejerea katiba yake ya zamani na anapendekeza katiba ya JMT ndio irekebishwe ili iendane na katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, kwake yeye shivji katiba ya Zanzibar ni kuu kuishinda ya JMT na ndio maana akashauri irekebishwe ili kuendana na matakwa ya katiba ya Zanzibar!!! Upunguaji wa mamlaka ya mahakama ya rufani; Hii shivji anakubali kuwa ni kweli ni kinyume cha katiba ila yeye binafsi anaona kuwa ni jambo dogo lisilostahili kukuzwa na halihatarishi muungano; Hivi wadau ni kweli kitendo cha mahakama ya Zanzibar kupiga maruku baadhi ya kesi zake kusikilizwa na mahaka ya rufani ya Tanzania, huku ukijulikana wazi kuwa mahaka ya rufani ni jambo la muungano, hakuhatarishi muungano? Katika sehemu ya hitimisho lake, anaongea kirahisi tu kuwa suluhu ya mambo haya mazito ni kurkebisha katiba zote mbili, yeye anaona ni rahisi tu, hili linathibisha ukweli kuwa hajafanya utafiti, na hizi ni hisia zake tu!! Hoja nyingine mufilisi kabisa aliyohitimisha nayo ni ile ya kudai kuwa watanzania hawaijui Tanganyika, hivyo hakuna sababu ya kuifufua, hii ni hoja ya mtu aliyeishiwa hoja, ambae ameanza kuokoteza hoja zisizo na msingi!! Hebu tujirejeshe kidogo kuitazama Nadharia ya Muungano. Hoja za muudo wa serikali zinatafsiriwa na sababu kuu mbili ambazo ni hoja za kisheria na hasira za kisiasa. 1.HOJA ZA KISHERIA Hoja za kisheria ni kwamba zinapoungana serikali mbili ni lazima pawepo na katiba ya serikali moja au tatu na wala sio mbili tena kisheria.Kwa mfano ni kwamba tume zote mbili zilizoundwa na Rais chini ya wasomi wa kisheria chini ya JAJI FRANSISI NYALALI na ile ya JAJI ROBERT KISANGA zote zilipendekeza serikali 3 na sio mbili. Kwa mfano endapo utampa msomi wa kisheria kazi ya kukuandalia katiba ya serikali mbili zinazotakiwa kuungana atakuandalia katiba ya serikali ama 1 au 3 lakini sio mboli kwani hazipo kisheria. 2.HASIRA ZA KISIASA Hasira za kisiasa ni sababu nyingine ya kuwa na serikali tatu,Kwa mfano mwaka 1984 aliyekuwa rais wa Zanzibar ABDU JUMBE aliasisi hoja ya kuwa na serikali 3 na ikamgharimu kunyang'anywa kadi ya CCM na kupoteza urais wa Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na MZEE ALI HASAN MWINYI 1984-1985 kabla ya kuchukuliwa na IDRISA ABDUL WAKIL 1985-1990. Mwaka 1993 paliibuka kundi la G55 liliokuwa na nia ya kuifufua Tanganyika kundi ambalo lilipelekea baraza la mawaziri kuvunjwa mwaka 1994 na baadhi ya mawaziri akiwemo waziri mkuu na makamu wa kwaza wa Rais kupoteza wadhifa wake. Mwaka huo huo 1993 Zanzibar ilitaka kujiunga na OAC wakakataliwa kwamba hawana mamlaka ya kufanya hivyo ndipo aliyekuwa Rais wa wakati huo DR SALIMIN AMOUR JUMA akasema Zanzibar imedharauliwa na kuzidi kupandisha homa na hasira za Wazanzibar kudai mamlaka kamili ya Zanziabar. Hata mwalimu Nyerere alikuwa na nia kwamba waunde serikali moja lakini kwa kuanzia alipendekeza kwamba waanze na serikali mbili ili wazanzibar wasiseme wamemezwa japo baadae alishindwa kuunda serikali moja. Kwahiyo hizo ndio sababu za mkanganyiko uliopo Tanzania katika mchakato wa katiba mpya

Share and Enjoy:

0 comments for this post

Leave a reply

Pata Habari papo kwa hapo
Weka anuani pepe yako hapa ili upate habari punde tunapo ziweka katika EAfrican Blog!
Subscribe via RSS Feed subscribe to feeds
wadhamini
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Popular Posts
Recent Stories
Ukurasa wetu wa Facebook
Wadhamini
Search
Archives
Blog Archives
Recent Comments
Tag Cloud