Home » ''Habari Zilizopewa Uzito'' »
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA MH. SAMWELI SITTA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI JIJINI DAR ES LAAM.
Mhe. Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba akimkaribisha Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta leo jijini Dar es Salaam wakati alipomtembelea kumuelezea maendeleo ya vikao vya Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Bakwata kuelezea maendeleo ya cikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bakwata Suleiman Lolila.(PICHA ZOTE NA BUNGE MAALUM LA KATIBA).
Na. Benedict Liwenga-Maelezo
MWENYEKITI wa Bunge maalum la Katiba Samweli Sitta amesema katiba mpya ni kwa manufaa ya wanachi wote kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam alipokutana na Mhe. Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba katika Ofisi za Bakwata zilizoko Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kwa ajili ya kuwashirikisha Viongozi wa madhehebu na dini ili nao wapate taarifa ya maendeleo ya bunge la katiba.
Mhe. Sita amesema kuwa Viongozi wa dini ni watu muhimu sana kwakuwa wanabeba wafuasi wengi katika jamii na kuwepo kwao kunasaidia katika maendeleo ya nchi hususani kujenge Amani ya nchi yetu na kuwahamasisha wananchi kuwa wavumilivu, watulivu, waelewa na wenye kupenda Amani.
Namuomba Mhe. Mufti pamoja viongozi wengine wa dini waizidi kutuombea ili tuweze kufikia muafaka katika kupata katiba mpya na bora yenye kuleta mabadiliko katika nch yetu” Alisema Mhe. Sitta.
Mhe. Sita Ameongeza kuwa Watanzania wanataka katiba itakayoijenga Taasisi imara zitakazoweza kusimamia mambo muhimu na kuweza kuondokana na uhalifu ikiwemo janga la madawa ya kulevya ambalo limekuwa likiisumbua sana nchii kwa msaada wa sheria mpya janga hili linawezekana kudhibitiwa.
Pia amewaomba wajumbe wa kamati kumi na mbili za bunge la katiba,wasome kwa makiini ibala ya sura ya 1 na ya 6 ambazo ni muhimu sana katika kuijenga nchi, ili waweze kutoka na mawazo mazuri na yakinifu kwa manufaa ya nchi na watu wake na kuweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo.
“Katiba itunge sheria ambazo ni imara zenye kufuata kanuni na taratibu dhabiti ili kuleta mabadiliko katika kuiongoza nchi na kuweza kuwasaidia wananchi wake” Alisema Mhe. Sitta.
Aidha, ameongeza kuwa Bunge hilo maalum linatarajia kuhailishwa mwezi wa nne tarehe 28 kwa ajili ya kupisha bunge la Bajeti,na kwa kuwa siku 70 hazitoshi kumaliza bunge hilo amemuomba Mheshimiwa Rais Kuwaongezea muda hivyo wanatarajia kurudi tena mwezi wa nane kuweza kuendelea na mijadala ya katiba mpya.
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more great content just like it.
Popular Posts
-
Na Yericko Nyerere (Mwanahalisi Forum) Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu a...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Muss...
-
Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambaye T...
-
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na ku...
-
THE Monduli Constituency MP, Edward Lowassa (b. Aug. 26,1953), has been causing a political storm of gargantuan proportions across the Tan...
-
Teller Ref No. UTT -MFI/TL/0414/15 Company:UTT Microfinance Plc Location:Dar Es Salaam POSITION DESCRIPTION: The UTT Microfinance Plc now i...
-
The jet, christened ‘The Great Rift Valley’ is the first of six 787s which Kenya Airways has ordered as part of its mordernisation ...
-
A list of famous people, chosen mainly from the Ninenteenth, Twentieth or Twenty First Century. This list includes famous actors, politici...
-
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimestushwa na kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuivunja mapema Tume ya Mabadiliko ya Katiba n...
Kuhusu sisi
Powered by Blogger.
Recent Stories
Ukurasa wetu wa Facebook
Wadhamini
Blog Archives
Recent Comments
Tag Cloud





0 comments for this post
Leave a reply