"Habari zilizopewa uzito"
Habari Mbali mbali

MNYIKA ASIKITISHWA NA MAJIBU YA MKUU WA MKOA WA DAR KUHUSU BODABODA NA BAJAJI



MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ameeleza kutoridhishwa na majibu yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, kuhusu mgogoro unaoendelea juu ya usafiri wa pikipiki ‘bodaboda’ na bajaj

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amenukuliwa na vyombo vya habari akisema hawezi kusitisha kwa muda agizo lake la kukataza vyombo hivyo vya usafiri kuingia katikati ya jiji kwa kuwa si agizo lake bali ni sheria.
Mnyika alisema jana kuwa mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo kutokana na kumuandikia ujumbe, akimtaka asitishe kwa muda utekelezaji wa tamko lake, ili kupisha mazungumzo kati ya serikali, wahusika wa bodaboda, bajaj na wadau wengine.“Nimepitia sheria inayohusika ambayo ni The Surface and Marine Transport Regulatory Authority Act, Sheria namba 9 ya mwaka 2001, hakuna kifungu chochote kinachokataza pikipiki au bodaboda na bajaj kuingia katika maeneo ya katikati ya jiji, hivyo mkuu wa mkoa anapaswa kutoa ufafanuzi kwa umma ni sheria ipi anaitumia,” alisema Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.Alisema Sadiq anapaswa kuzingatia kwamba sheria hiyo kifungu cha 5 imetamka kwamba wajibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ni kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma na kuhamasisha upatikanaji wa huduma, ikiwemo kwa wateja wa kipato cha chini.“Usafiri wa pikipiki/bodaboda na bajaj sio tu umetoa fursa ya ajira kwa vijana, bali pia unasaidia wananchi wa kipato cha chini na pia unasaidia katika mazingira ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam, hivyo agizo la kutaka usafiri huo uishie Buguruni, Ubungo, Tazara na Chuo cha Uhasibu ni suala ambalo limeibua mgogoro unaostahili ufumbuzi wa haraka,” alisema Mnyika.
Pia aliongeza ili fedha za umma ziweze kutumika vizuri, katika barua yake ya kupendekeza ajenda, atapanua wigo wa mjadala wa matatizo ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam ili masuala yote ya kisheria yaweze kujadiliwa na maazimio ya utekelezaji kuweza kupangwa.Mbunge huyo ameongeza kuwa tayari ameshawaandikia ujumbe wabunge wenzake wa Dar es Salaam, waweze kuunga mkono ajenda hiyo kujadiliwa na ufumbuzi uweze kupatikana kwa maslahi ya vijana na wasafiri katika jiji hilo.

Share and Enjoy:

0 comments for this post

Leave a reply

Pata Habari papo kwa hapo
Weka anuani pepe yako hapa ili upate habari punde tunapo ziweka katika EAfrican Blog!
Subscribe via RSS Feed subscribe to feeds
wadhamini
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Popular Posts
Recent Stories
Ukurasa wetu wa Facebook
Wadhamini
Search
Archives
Blog Archives
Recent Comments
Tag Cloud