"Habari zilizopewa uzito"
Habari Mbali mbali

Yanga yawapa kadi nyekundu wanne

KATI ya mechi tisa ambazo Yanga imecheza kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, michezo yao minne iliwasababishia baadhi ya wachezaji wa timu pinzani watolewe kwa kadi nyekundu.
Yanga imebakiza mechi nne mkononi dhidi ya Kagera Sugar, JKT Oljoro, JKT Ruvu na Simba.
Timu ambazo ziliwapoteza wachezaji wao kwa kadi nyekundu ni Mtibwa Sugar ambayo mshambuliaji wake, Abdallah Juma, alitolewa kwa kadi nyekundu katika mechi iliyochezwa mjini Morogoro ambapo timu hizo hazikufungana.
Azam FC ilimpoteza beki wa kulia, Erasto Nyoni baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Yanga alifungwa mabao 2-1.
Sekeseke hilo, limewakuta pia Mgambo Shooting Jumapili iliyopita walipoifunga Yanga mabao 2-1, mshambuliaji wao Mohamed Neto alipewa kadi nyekundu.
Mchezaji mwingine ni Steven Mazanda wa Mbeya City, yeye alionyeshwa kadi nyekundu na timu yake ikafungwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mechi za Yanga ambazo wapinzani wao walitoka salama kwenye mzunguko huu wa pili ni dhidi ya Coastal Union walipocheza Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakashindwa kufungana.
Mechi nyingine waliifunga Ashanti mabao 2-1 jijini Dar es Salaam, walipoishinda Rhino nyumbani kwao Tabora mabao 3-0. Pia katika ushindi wa Yanga wa mabao 5-0 walipoifunga Prisons Mbeya na walipoipiga Ruvu Shooting mabao 7-0 Uwanja wa Taifa.
Kocha mzawa, Kenny Mwaisabula, ametoa ufafanuzi wa kitaalamu wa suala hilo na kusema: “Hii ni kwa sababu Yanga wana wachezaji wenye kasi na inajulikana kuwa inao washambuliaji wazuri.
“Kwa maana hiyo, ili kuidhibiti kasi ya wachezaji kama Msuva (Simon), Ngassa (Mrisho), Okwi (Emmanuel) au Kiiza (Hamis) ni lazima uwachezee faulo ambazo ndiyo zinazalisha kadi nyekundu.
“Kwa kawaida, mabeki huwa hawataki kufungwa na ndiyo maana mambo kama hayo yanatokea.”
Yanga ni ya pili kwenye msimamo wa ligi, ina pointi 46, wakati Azam ndiyo inaongoza kwa pointi 53. Mbeya City ni ya tatu ina pointi 45 wakati Simba ni ya nne inazo 36.

Share and Enjoy:

0 comments for this post

Leave a reply

Pata Habari papo kwa hapo
Weka anuani pepe yako hapa ili upate habari punde tunapo ziweka katika EAfrican Blog!
Subscribe via RSS Feed subscribe to feeds
wadhamini
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Designed by Cebanet.netDesigned by Cebanet.netDesigned by Cebanet.net
Popular Posts
Recent Stories
Ukurasa wetu wa Facebook
Wadhamini
Search
Archives
Blog Archives
Recent Comments
Tag Cloud