MWENDELEZO WA THAMTHILIYA YA TANZANIA NA KATIBA MPYA
Tanzania na katiba mpya ni mwendelezo wa tamthiliya inayochezwa
makusudi kama ghiliba kwa wananchi,nachelea kusema hivyo kutokana na mchakato huo umejikita kimakundi zaidi na kusahau matakwa na mawazo ya walio wengi kwa kupuuzwa na kujali maslahi ya wachache.
Rais ni alama ya utaifa ndani ya JMT lakini akitumika kama kiongozi wa chama na kusahau dhamana aliyopewa ya urais kama taasisi hapo ndipo mchakato huu unaogeuka kuwa tamthiliya.
Leo kila Mtanzania amewekwa njia panda kutokana na hali hii ya mchakato huu wa katiba kugeuzwa ni agenda ya kichama zaidi na si ya Watanzania.Rais anapoingilia na kuiponda tume iliyokuwa inampaa taarifa kila mara inaonyesha jinsi gani upoteshaji wa makusudi unaopofanywa makusudi.
Kwanza utaona mchakato huu umekiukwa kwa kanuni zake kuvunjwa na kumpa rais nafasi ya kumjibu Jaji Warioba na tume ya rais ya kuratibu na kuandaa rasimu ya katiba.Kanuni ilizungumza wazi kuwa akishaapishwa M/kiti rais atazindua bunge na Jaji Warioba kama M/Kiti wa tume ya katiba atawasilisha mezani rasimu hiyo.
Kilichofanyika ni kiini macho ambacho kwa makusudi kabisa M/kiti wa bunge maalumu aliamua kuvunja kanuni na kumtaka M/kiti wa tume awasilishe karatasi mezani kabla bunge halijazinduliwa na kumpa nafasi ya kuzindua bunge, rais aliyeligeuza bunge kuwa party caucus ya CCM kwa kuijibu tume aliyoiunda yeye mwenyewe huku akijulishwa kila hatua iliyokuwa imefikia.
Ni tamthiliya kwa kuwa kilichofanyika kutoka kwa M/kiti wa bunge hili maalumu ni mwendelezo wa kiini macho ambacho hakijawahi kutokea duniani.Mathalani uchaguzi mkuu umefanyika,wabunge wamechaguliwa wakaapishwa,kabla rais hajazindua bunge hoja zinawakilishwa mezani na rais ndipo ana zindua bunge,uliona wapi hiyo!
Uko wapi umakini wa bunge hili maalumu ikiwa limeanza makosa ya makusudi kwa M/kiti huyu kuvunja kanuni zilizotungwa na bunge hili ili tu kufunika kombe mwanaharamu apite!
Ikiwa mwanzo tumeanza kwa kuchakachua mwisho wake tunategemea kupata katiba ya JMT au ni maboresho ya katiba ya CCM!
Sheria nyingine iliyotungwa ya kusimamia mjadala wa rasimu ya katiba iliyoko bungeni hivi sasa inatamka wazi kuwa bunge hili maalumu halitakuwa na mamlaka ya kubadilisha chochote ndani ya rasimu isipokuwa tu kuboresha na si kuipotosha.
Anapokuja rais na kuligeuza bunge NEC ya CCM kwa kutoa tamko na msimamo wa chama chake kuwa wao ni serikali mbili na kujibu hoja kwa kupinga takwimu na yeye kupika akwimu zake ili kupata ushawishi kwa wateule wake na wafuasi wa chama chake ni ukiukwaji wa makusudi wa sheria inayotamka wazi kutokubadili bali kukiboresha kilichoko ndani ya rasimu.
Imekuwa ni kawaida sasa kwa taasisi ya urais kutumika vibaya katika kusimamia mabaya yote yanayofanywa na serikali hii kwa kuliongopea taifa makusudi kwa minajili ya maslahi ya wachache kiasi cha kutaka kuuteka mjadala huu na kuwa wa CCM zaidi kwa kupitisha wayatakayo wao kama chama na kudharau yale yote waliyoyataka wananchi.
Wabunge wa JMT wakati wanatunga sheria zitazoendesha mchakato wa rasimu ya katiba walisimama kiushabiki zaidi kwa kutunga sheria walizoziona kuwa zitakuwa na maslahi kwao,lakini sheria hizo hizo walizotnga zimegeuka kuwa shubiri na kuamua kuzikiuka kwa makusudi.
Kuna mambo mengi ya msingi kama taifa ambayo rais anayakana wazi kuwa hayastahili kuingia kwenye katiba kama vile mambo yahusuyo kilimo.Lakini ana sahau mgogoro mkubwa ndani ya nchi hii ni ardhi na kilimo kwa kuwa serikali haina sera nzuri za kilimo zaidi ya uzuri wa kauli mbiu zisizo na mashiko katika utekelezaji wake.Hakuna mfumo mzuri unaoainisha kilimo kionekane kuwa uti wa mgongo wa taifa hili kwa kuundiwa sheria ndani ya katiba hii mpya ili kuepuka utii huu wa mgongo wa taifa hili kuchezewa na wanasiasa makanjanja.
Kuna haja sasa kwa Watanzania wenzangu kukataa makusudi maigizo yanayoendelea huko Dodoma kwa sehemu ya tatu ya tamthiliya hii mpya ya Tanzania na katiba mpya haijaanza ili kupinga matumizi mabaya ya rasilimali muda na kodi za Watanzania huku kilichotegemewa na wengi kikipuuzwa na kujaribu kutengenezwa kipya zaidi ambacho hakitokani na matakwa ya walio wengi(Watanzania).
Ni bora basi rais wa JMT angemwita rais wa dola kamili ya SMZ wakajifungia chumbani na kupitisha yale ya kwao kwa maslahi ya chama chao kuliko kupoteza muda na pesa za Watanzania kutafuta ridhaa ya wengi ili kunufaisha maslahi ya wachache.
Rais bado ana nafasi ya kuisafisha dhamira yake na kutanguliza maslahi ya Watanzania mbele,aepuke anachokisema mbali na anachokitenda mbali kama alivyowaasa wanasiasa watangulize maslahi ya taifa mbele kwa kujadili maslahi mapana zaidi ya taifa na watu wake.Bado ana nafasi ya kuwaomba radhi wananchi ili ile dhana ya ulevi wa madaraka impitie
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more great content just like it.
-
Na Yericko Nyerere (Mwanahalisi Forum) Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu a...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Muss...
-
Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambaye T...
-
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na ku...
-
THE Monduli Constituency MP, Edward Lowassa (b. Aug. 26,1953), has been causing a political storm of gargantuan proportions across the Tan...
-
Teller Ref No. UTT -MFI/TL/0414/15 Company:UTT Microfinance Plc Location:Dar Es Salaam POSITION DESCRIPTION: The UTT Microfinance Plc now i...
-
The jet, christened ‘The Great Rift Valley’ is the first of six 787s which Kenya Airways has ordered as part of its mordernisation ...
-
A list of famous people, chosen mainly from the Ninenteenth, Twentieth or Twenty First Century. This list includes famous actors, politici...
-
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimestushwa na kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuivunja mapema Tume ya Mabadiliko ya Katiba n...




0 comments for this post
Leave a reply