MJADALA WA RASIMU YA KATIBA SURA YA KWANZA NA SITA
Wadau, amani iwe kwenu. ..,
Kwa mujibu wa Ratiba ya vikao vya Bunge Maalum ambapo nimepata nakala yake, ni kwamba kuanzia juzi tarehe 31 Machi 2014, Bunge Maalum limeanza vikao vya kujadili vifungu vya Rasimu ya Katiba kupitia kwenye mijadala ya Kamati za Bunge Maalum. Mijadala hiyo itahitimishwa Jumamosi tarehe 12 Aprili 2014 ambapo Bunge Maalum litapiga kura kufanya maamuzi juu ya vifungu hivyo. Mijadala hiyo kwa mujibu wa vifungu hivyo inahusu Sura ya Kwanza na ya Sita. Zimechaguliwa sura mbili ili kukidhi matakwa ya kikanuni. Aidha, Wamechagua sura ya Sita badala ya Sura ya Kwanza na ya Pili si kwa vile Mwenyekiti anaitwa Sammuel Sita na hivyo kupendekeza sura ya sita ianze kwa lengo la kulipa heshima jina lake, la hasha. Sura hizo mbili zimeteuliwa na Kamati ya Uongozi kutokana na umuhimu wake. Kwani sura hizo mbili zinahusu hatima ya nchi yetu. Pia sura hizo ndizo sura mama za Rasimu ya Katiba hivyo ni vema zikajadiliwa kwanza ili maamuzi yatakayofikiwa juu ya sura hizo ndiyo yatakayotoa muelekeo wa mjadala mzima wa Rasimu ya Katiba.
Mjadala mkubwa utakaoibuka kwenye Kamati na kwenye vikao vya Bunge Maalum unatarajiwa kuwa ni juu ya muundo wa muungano. Hapa tunatarajia kuwa na mjadala mkali na wakati mwingine wabunge watapandwa na jazba hali itakayowapelekea kukiuka baadhi ya kanuni za Bunge Maalum. Watafanya hivyo kwa lengo la kutetea misimamo yao kuhusu muundo wa muungano. Kwa hali ilivyo hivi sasa, mchuano mkali ni baina ya wale wanaotaka muundo wa Serikali Mbili kama ilivyo kwenye Katiba iliyopo na wale wanaotaka muundo wa Serikali Tatu kama ulivyoainishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Naamini kuwa hata humu ndani ya mitandao ya kijamii pia watu tumegawanyika kwa muktadha huo. Pia naamini kuwa kuna waumini wa serikali Moja na Serikali Nne. Yote hayo ni mawazo ya wabunge na wananchi. Hata hivyo mwisho wa siku ni kwamba ni muundo mmoja tu ndio utakaopitishwa tarehe 12 Aprili 2014 kwa kura ya wazi na siri kutegemeana na utashi wa mbunge.
kwa lengo la kupanuana mawazo juu ya mjadala huu, nawaalika wachambuzi mbalimbali ambao wataweka hoja za msingi hasa juu ya muundo wa muungano. Watu tujadili kwa hoja na si kuendekeza ushabiki wa kisiasa. Wachangiaji ni vema tukajikita kwenye hoja. kejeli na dharau dhidi ya aina fulani ya muungano na wafuasi wake hazitasaidia kwenye mjadala huu. Pia wachambuzi ambao watasimama kati kwa kati watatusaidia sana kupata mawazo ya pande zote mbili kwa ufasaha. Wale watakaoamua kuweka bayana misimamo yao wanapaswa pia kueleza kwa nini wanaona kuwa muundo wanaoupendekeza ni bora zaidi. Naomba Kuwasilisha.....


Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more great content just like it.
-
Na Yericko Nyerere (Mwanahalisi Forum) Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu a...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Muss...
-
Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambaye T...
-
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na ku...
-
THE Monduli Constituency MP, Edward Lowassa (b. Aug. 26,1953), has been causing a political storm of gargantuan proportions across the Tan...
-
Teller Ref No. UTT -MFI/TL/0414/15 Company:UTT Microfinance Plc Location:Dar Es Salaam POSITION DESCRIPTION: The UTT Microfinance Plc now i...
-
The jet, christened ‘The Great Rift Valley’ is the first of six 787s which Kenya Airways has ordered as part of its mordernisation ...
-
A list of famous people, chosen mainly from the Ninenteenth, Twentieth or Twenty First Century. This list includes famous actors, politici...
-
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimestushwa na kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuivunja mapema Tume ya Mabadiliko ya Katiba n...



0 comments for this post
Leave a reply